Kusikiliza na Kuzungumza
1.1 Kusikiliza na Kujibu Mjadala
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika kusikiliza mjadala
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika kuchangia mjadala
- kushiriki mjadala kwa kuzingatia vipengele vifaavyo katika kusikiliza na kuchangia mijadala
- kuchangamkia kushiriki katika mijadala ya miktadha mbalimbali
- Je, unazingatia nini wakati wa kusikiliza na kuchangia mjadala?
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika kusikiliza mjadala
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika kuchangia mjadala
- kusikiliza au kutazama mjadala kuhusu suala lengwa katika kifaa cha kidijitali
- kueleza vipengele vya kusikiliza na kuchangia mjadala vilivyozingatiwa katika mjadala aliosikiliza
- kushiriki mjadala kuhusu suala lengwa akiwa na wenzake akizingatia vipengele vifaavyo vya mjadala
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.2 Kusikiliza kwa Kina Sauti /b/ na /mb/
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutamka sauti /b/ na /mb/ ipasavyo ili kuzitofautisha kimatamshi
- kutamka vitanzandimi vyenye sauti /b/ na /mb/ ipasavyo
- kuunda vitanzandimi vyepesi vyenye sauti /b/ na /mb/
- kuchangamkia matamshi bora ya sauti /b/ na /mb/ katika mazungumzo ya kawaida
- Kutamka maneno yenye sauti /b/ na /mb/ ipasavyo kuna umuhimu gani?
- kutambua sauti /b/ na /mb/ katika maneno na vifungu
- kusikiliza na kutamka vitanzandimi vyepesi vinavyohusisha matamshi ya sauti /b/ na /mb/ katika kifaa cha kidijitali kama vile simu, redio
- kubuni vitanzandimi vyepesi vinavyohusisha sauti /b/ na /mb/
- kuwasomea wenzake vitanzandimi alivyobuni ili wamtolee maoni
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.3 Semi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya tashbihi, sitiari na methali ili kuzipambanua
- kutambua tashbihi, sitiari na methali katika matini ya fasihi simulizi
- kueleza matumizi ya tashbihi, sitiari na methali katika matini ya fasihi simulizi
- kutumia tashbihi, sitiari na methali katika uwasilishaji wa tungo za fasihi simulizi
- kuchangamkia matumizi ya tashbihi, sitiari na methali katika tungo za fasihi simulizi
- Tunatumia mbinu gani za lugha katika kuwasilisha tungo za fasihi simulizi?
- Kwa nini tunatumia tashbihi, sitiari na methali kuwasilisha tungo za fasihi simulizi?
- kueleza maana ya tashbihi, sitiari na methali
- kutambua tashbihi, sitiari na methali kutoka kwenye tungo simulizi, kapu la semi, au kifaa cha kidijitali
- kutumia vifaa vya kidijitali kusakura matumizi ya tashbihi, sitiari na methali katika tungo za fasihi simulizi
- kujadili na mwenzake matumizi ya tashbihi, sitiari na methali alizotafiti mtandaoni
- kushiriki katika uwasilishaji wa tashbihi, sitiari na methali
- kujadiliana na mzazi au mlezi wake kuhusu tashbihi, sitiari na methali katika jamii yake
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.4 Semi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya vitendawili na nahau ili kuipambanua
- kutambua vitendawili na nahau katika matini
- kufafanua umuhimu wa vitendawili na nahau katika fasihi simulizi
- kutumia nahau ipasavyo katika mawasiliano
- kuwasilisha vitendawili kwa kuzingatia vipengele vya uwasilishaji wake
- kuchangamkia matumizi ya nahau na uwasilishaji wa vitendawili katika tungo za fasihi
- Unazingatia nini unapowasilisha vitendawili?
- Kwa nini tunatumia nahau katika mawasiliano?
- kueleza maana ya vitendawili
- kueleza maana ya nahau
- kutambua vitendawili na nahau mbalimbali katika matini ya fasihi simulizi na kueleza maana zake
- kutafiti mtandaoni au maktabani umuhimu wa vitendawili na nahau
- kujaza nafasi katika sentensi kwa kutumia nahau mwafaka
- kutunga sentensi kwa kutumia nahau ipasavyo
- kujadili vipengele vya uwasilishaji wa vitendawili akiwa na wenzake
- kuwawasilishia wenzake vitendawili kwa kuzingatia vipengele vya uwasilishaji wa vitendawili
- kushirikiana na mzazi au mlezi wake kutambua vitendawili na nahau katika jamii yake
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.5 Ufahamu wa Kusikiliza
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya ufahamu wa kusikiliza
- kujadili kanuni za ufahamu wa kusikiliza
- kujadili vipengele vya ufahamu wa kusikiliza
- kushiriki katika ufahamu wa kusikiliza akizingatia vipengele vyake
- kuchangamkia kushiriki katika kusikiliza kwa ufahamu ili kukuza stadi ya kusikiliza
- Je, ni mambo gani unayozingatia ili kupata ujumbe unaposikiliza matini?
- Je, kusikiliza kwa ufahamu kuna faida zipi?
- kueleza maana ya ufahamu wa kusikiliza
- kujadili na wenzake kanuni za ufahamu wa kusikiliza
- kujadili na wenzake vipengele vya ufahamu wa kusikiliza
- kusikiliza ufahamu kuhusu suala lengwa kutoka kwa mwalimu au mgeni mwalikwa na kujibu maswali
- kusikiliza matini kuhusu suala lengwa katika chombo cha kidijitali na kujibu maswali
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.6 Kusikiliza kwa Kufasiri
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya kusikiliza kwa kufasiri ili kuibanisha
- kueleza msimamo na mielekeo kuhusu ujumbe wa matini ya kusikiliza
- kulinganisha misimamo na mielekeo ya ujumbe wa matini aliyosikiliza na ile ya jamii yake kuhusu suala husika
- kujenga mazoea ya kutambua msimamo na mielekeo katika matini mbalimbali ili kupata maana ya ujumbe
- Ni misimamo gani iliyopo katika matini ulizowahi kuzisikiliza?
- kutafiti mtandaoni au maktabani maana ya kusikiliza kwa kufasiri na kuwasilisha matokeo ya utafiti wake darasani ili apate maoni ya wenzake
- kueleza misimamo na mielekeo kuhusu ujumbe katika matini anayosikiliza kuhusu suala lengwa
- kusikiliza habari kuhusu suala lengwa (miongozo kwa watumiaji wa barabara; wanaotumia usafiri wa shuleni ulioidhinishwa) katika kifaa cha kidijitali na kuchambua misimamo na mielekeo kuhusu ujumbe
- kulinganisha misimamo na mielekeo kuhusu ujumbe wa matini aliyosikiliza na misimamo na mielekeo ya jamii yake kuhusu suala lililozungumziwa katika matini hiyo
- kutoa muhtasari wa habari aliyosikiliza kuhusu suala lengwa huku wakichanganua misimamo na mielekeo ya msimulizi /msemaji kuhusu masuala yanayozungumziwa
- kuwaeleza wenzake misimamo na mielekeo kuhusu ujumbe katika matini aliyosikiliza kwa maneno yake mwenyewe na kuwataka waangazie vipengele vilivyotumiwa kuonyesha misimamo na mielekeo hiyo
- kujadili na mzazi au mlezi wake kuhusu misimamo na mielekeo ya jamii yake kuhusu suala lengwa
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.7 Kusikiliza kwa Kutathmini
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya kusikiliza kwa kutathmini ili kuibainisha
- kujadili vipengele vya kuzingatia katika kusikiliza kwa kutathmini
- kutathmini ujumbe wa mzungumzaji
- kutathmini mtazamo wa msemaji kuhusu anachokizungumzia
- kueleza maana ya msamiati kama ulivyotumiwa katika matini aliyosikiliza
- kuchangamkia kushiriki katika kusikiliza kwa kuchanganua ili kuboresha mawasiliano
- Unazingatia nini ili kupata ujumbe unaowasilishwa na mzungumzaji?
- kueleza maana ya kusikiliza kwa kutathmini ili kuubainisha
- kujadili na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kusikiliza kwa kutathmini kutoka kwenye mazungumzo mafupi
- kusikiliza mazungumzo kuhusu suala lengwa (k.v Majukumu ya Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama Barabarani, Kituo cha Huduma kwa Taifa,) kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au katika vifaa vya kidijitali huku akijadili vipengele vya kusikiliza kwa kutathmini vilivyozingatiwa
- kutoa maoni kuhusu suala linaloshughulikiwa katika kauli au kifungu alichosikiliza
- kusikiliza matini kuhusu suala lengwa kutoka kwenye kinasa sauti au kwa mgeni mwalikwa na kueleza maana ya msamiati ambao umetumiwa katika matini hiyo
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.8 Uzungumzaji wa Kushawishi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya uzungumzaji wa kushawishi ili kuupambanua
- kubainisha miktadha ya uzungumzaji wa kushawishi
- kujadili vipengele vya kuzingatia katika uzungumzaji wa kushawishi
- kufanya mazungumzo ya kushawishi akizingatia vipengele vya uzungumzaji wa kushawishi
- kujenga mazoea ya kuwasilisha hoja kwa mazungumzo yanayoshawishi hadhira
- Ni lini tunatumia mazungumzo ya kushawishi?
- Utafanya nini ili mazungumzo yako yawe na ushawishi kwa wengine?
- kutafiti na kueleza maana ya uzungumzaji wa kushawishi
- kubainisha, miktadha katika jamii yake ambamo uzungumzaji wa kushawishi hutokea
- kushirikiana na wenzake kujadili vipengele vya kuzingatia katika uzungumzaji wa kushawishi
- kubuni mazungumzo mepesi kuhusu suala lengwa na kuwawasilishia wenzake wamtathmini iwapo ametumia vipengele vifaavyo vya uwasilishaji wa uzungumzaji wa kushawishi
- kusikiliza uzungumzaji wa kushawishi kuhusu suala lengwa kutoka kwenye kifaa cha kidijitali au mgeni mwalikwa na kubainisha vipengele vya uzungumzaji wa kushawishi vilivyozingatiwa
- kushirikiana na wenzake katika uzungumzaji wa kushawishi kuhusu suala lengwa huku akizingatia vipengele vya uwasilishaji wa uzungumzaji wa kushawishi
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.9 Kusikiliza kwa Kina Sauti /j/ na /nj/
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua sauti /j/ na /nj/ katika maneno
- kutamka maneno yenye sauti /j/ na /nj/ ipasavyo
- kubuni vitanzandimi vinavyohusisha sauti /j /na /nj/
- kuchangamkia matamshi bora ya sauti /j/ na /nj/ ili kufanikisha mawasiliano
- Ni maneno yapi unayoyajua yaliyo na sauti /j/ na /nj/?
- kutambua sauti /j/ na /nj/ katika maneno
- kusikiliza vitanzandimi katika kifaa cha kidijitali na kutambua maneno yenye sauti /j/ na /nj/ na kuyatamka ipasavyo
- kutamka vitanzandimi vyepesi vinavyohusisha matamshi ya sauti/ j/ na /nj/
- kubuni vitanzandimi vinavyohusisha sauti /j/ na /nj/ na kuvikariri kwa wenzake
- kushiriki mazungumzo na mzazi au mlezi wake kwa kuzingatia matamshi bora ya sauti /j/ na /nj/
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.10 Mazungumzo Malumbano ya Utani
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya malumbano ya utani kama kipera cha mazungumzo
- kujadili sifa za malumbano ya utani
- kutambua vipengele vya uwasilishaji wa malumbano ya utani
- kuwasilisha malumbano ya utani kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya uwasilishaji
- kuchangamkia uwasilishaji wa malumbano ya utani kwa kuzingatia vipengele vya kimsingi katika uwasilishaji
- Malumbano ya utani huzungumzia nini?
- kutafiti na kueleza maana ya malumbano ya utani
- kutafiti na kujadili na wenzake sifa za malumbano ya utani
- kutambua vipengele vya kimsingi vya uwasilishaji wa malumbano ya utani
- kusikiliza malumbano ya utani katika vifaa vya kidijitali au kutoka kwa mgeni mwalikwa au mwalimu na kutambua vipengele vya kimsingi katika uwasilishaji
- kuwasilisha malumbano ya utani kwa kuzingatia vipengele vya kimsingi katika uwasilishaji wake
- kumweleza mzazi au mlezi jinsi ya kuwasilisha malumbano ya utani kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya uwasilishaji
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.11 Uzungumzaji katika Sherehe
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya uzungumzaji katika sherehe
- kutambua miktadha katika jamii ambapo uzungumzaji katika sherehe hufanywa
- kujadili ujumbe tofautitofauti unaoafiki uzungumzaji katika miktadha mbalimbali ya sherehe
- kujadili vipengele vya kuzingatia katika uzungumzaji katika muktadha wa sherehe
- kutoa mazungumzo katika muktadha wa sherehe kwa kutumia vipengele vifaavyo
- kuchangamkia mazungumzo yafaayo katika miktadha ya sherehe
- Ni mambo gani ya kuzingatia wakati wa kuzungumza katika muktadha wa sherehe?
- kueleza maana ya uzungumzaji katika sherehe
- kutambua miktadha katika kijamii yake ambamo uzungumzaji katika miktadha ya sherehe hufanywa
- kusakura katika mtandao kutafiti ujumbe unaoafiki uzungumzaji katika miktadha mbalimbali ya sherehe
- kusikiliza uzungumzaji wa aina mbalimbali kutoka kwenye vifaa vya kidijitali, mwalimu au mgeni mwalikwa na kubainisha ule unaohusu muktadha ya sherehe
- kutafiti na kujadili na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kuzungumza katika miktadha ya sherehe
- kuigiza uzungumzaji katika miktadha ya sherehe huku akizingatia vipengele vya uwasilishaji wa uzungumzaji wa aina hii
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.12 Ufahamu wa Kusikiliza Matini ya kusikiliza
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza habari katika matini ya kusikiliza
- kukadiria maana ya msamiati mahususi na vifungu katika matini ya kusikiliza
- kuchanganua mitazamo na maoni katika matini ya kusikiliza
- kufurahia kusikiliza matini za kusikiliza ili kupata habari mahususi
- Je, unazingatia nini ili kufanikisha ufahamu wa kusikiliza?
- kueleza hoja muhimu katika habari aliyosikiliza kuhusu suala lengwa kutoka kwa mwalimu, kifaa cha kidijitali, mgeni mwalikwa au wenzake
- kukadiria maana ya msamiati mahususi na vifungu katika matini ya kusikiliza
- kujadili na wenzake mitazamo na maoni katika kifungu cha kusikiliza
- kushirikisha mzazi, mlezi au mwenzake kusikiliza kifungu kutoka kifaa cha kidijitali na kujadili mitazamo katika kifungu hicho
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.13 Mazungumzo Mawaidha
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua vipengele vya lugha vinavyotumika katika mawaidha
- kujadili umuhimu wa vipengele vya lugha vinavyotumika katika mawaidha
- kujadili ishara zifaazo katika kutoa mawaidha
- kutoa mawaidha kwa kuzingatia vipengele mbalimbali vya lugha ya mawaidha na ishara zifaazo
- kuonea fahari utoaji wa mawaidha katika maisha ya kila siku
- Unazingatia nini unapotoa mawaidha?
- kutambua vipengele vya lugha kwa kusikiliza mawaidha yakitolewa na mwalimu, mwanafunzi mwenzake, mgeni mwalikwa au katika vifaa vya kidijitali
- kujadili umuhimu wa vipengele vya lugha vilivyotumika katika mawaidha aliyosikiliza akiwa na wenzake
- kujadili na wenzake ishara zifaazo katika kutoa mawaidha
- kutoa mawaidha kwa mwenzake yanayohusiana na matumizi ya ushuru akizingatia vipengele mbalimbali vya lugha
- kusikiliza mawaidha yakitolewa na mzazi au mlezi wake na kutambua vipengele vya lugha katika mawaidha hayo
- kusakura mtandaoni na kusikiliza mawaidha mbalimbali kisha atambue vipengele vya lugha katika mawaidha hayo kumweleza mzazi, mlezi au mwenzake vipengele vya lugha ya mawaidha
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
1.14 Kusikiliza kwa Kutathmini
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya kusikiliza kwa kutathmini
- kujadili vipengele vya kuzingatia katika kutathmini mazungumzo
- kusikiliza mazungumzo na kuyatathmini kwa kuzingatia vipengele vifaavyo
- kuchangamkia kutathmini mazungumzo ili kuimarisha mawasiliano
- Kusikiliza kwa kutathmini mazungumzo kuna umuhimu gani?
- Unazingatia nini katika kutathmini ufaafu wa mazungumzo?
- kutafiti na kueleza maana ya kusikiliza kwa kutathmini
- kujadili na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kutathmini mazungumzo kutoka kwenye mazungumzo mafupi
- kusikiliza mazungumzo kuhusu suala lengwa kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au kwenye vifaa vya kidijitali na kuyatathmini kwa kuzingatia vipengele mbalimbali
- kushiriki na mzazi au mlezi wake katika mazungumzo kuhusu suala lengwa na kutoa maoni kuhusu suala linalozungumziwa
Approved course books, concrete realia, charts, manipulatives & digital devices.
