Kusoma
1.1 2.1 Kusoma kwa Kina Tamthilia
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua mandhari na ploti katika tamthilia
- kueleza umuhimu wa mandhari na ploti ili kuubanisha
- kujadili mandhari na ploti ya tamthilia aliyosoma
- kuchangamkia nafasi ya mandhari na ploti katika tamthilia
- Ni mandhari gani unayokumbuka yaliyo katika tamthilia ulizowahi kusoma?
- Ploti ina umuhimu gani katika tamthilia ulizowahi kusoma?
- kutambua mandhari mbalimbali katika tamthilia akishirikiana na wenzake
- kueleza umuhimu wa mandhari katika katika tamthilia akishirikiana na wenzake
- kuandika kwa ufupi kuhusu mandhari katika tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu
- kuwawasilishia wenzake darasani uchambuzi wake kuhusu mandhari
- kusoma chapisho la tamthilia au kutoka mtandaoni na kutambua mandhari yake
- kutambua ploti ya tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu au kwa kushirikiana na wenzake
- kujadili umuhimu wa ploti ya tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu au na wenzake
- kuandaa muhtasari kuhusu ploti ya tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu
- kuwawasilishia wenzake darasani uchambuzi wake kuhusu ploti ya tamthilia aliyosoma
- kumweleza mzazi au mlezi kuhusu mandhari na ploti katika tamthilia aliyosoma
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.2 Kusoma kwa Ufahamu Kifungu cha Kushawishi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua habari mahususi katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi
- kutabiri matukio katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi
- kueleza maana ya msamiati na vifungu vya maneno katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi
- kujadili ushawishi katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi
- kuchangamkia usomaji wa ufahamu shawishi ili kukuza hamu ya ujifunzaji
- Ni kwa njia gani tunaweza kutambua ujumbe wenye lengo la kushawishi katika habari?
- kusoma ufahamu wa kifungu cha kushawishi kutoka kwa vitabu au vifaa vya kidijitali na kudondoa habari mahususi (k.v. nani, nini, wapi, lini)
- kutabiri matukio katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi akishirikiana na wenzake
- kueleza maana ya msamiati kuhusu suala lengwa (k.v. maneno na nahau) katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi na kuueleza kwa kutumia kamusi akishirikiana na wenzake
- kujadili ushawishi katika kifungu cha ufahamu akishirikiana na wenzake
- kuwawasilishia wenzake kazi yake ili wamtolee maoni
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.3 Kusoma kwa Kina Wahusika katika tamthilia
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua wahusika katika tamthilia aliyosoma
- kujadili sifa za wahusika katika tamthilia
- kujadili mafunzo yanayotokana na wahusika katika tamthilia
- kujenga mazoea ya usomaji wa kazi za kifasihi ili kukuza hamu ya ujifunzaji
- Ni mambo yapi yanayokuelekez a kuwaelewa wahusika katika tamthilia?
- Je, ni mambo gani tunayoweza kujifunza kutokana na wahusika wa tamthilia?
- kutambua wahusika katika tamthilia aliyoisoma
- kujadili na wenzake sifa za wahusika katika tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu
- kuigiza wahusika katika tamthilia akiwa na wenzake ili kukuza uelewa wa sifa zao
- kueleza uhusiano kati ya wahusika katika tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu
- kutazama video kuhusu wahusika katika tamthilia aliyosoma
- kuandaa muhtasari kuhusu sifa za wahusika katika video aliyotazama
- kujadili mafunzo yanayotokana na matendo ya wahusika akishirikiana na wenzake
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.4 Kusoma kwa Mapana Matini ya kujichagulia
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kuteua matini ifaayo ya kujisomea
- kueleza ujumbe katika matini ya kujichagulia
- kutambua maana za msamiati na matumizi mengine ya lugha katika matini ya kujichagulia
- kujenga mazoea ya kusoma matini mbalimbali katika maisha ya kila siku
- Unavutiwa zaidi na nini unaposoma makala ya kujichagulia?
- Unazingatia mambo gani wakati wa kusoma makala ya kujichagulia?
- kuteua matini ifaayo ya kujisomea
- kueleza ujumbe wa matini ya kujichagulia aliyoisoma
- kutambua msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia (k.v. ya usalama barabarani (mfano; tabia hatarishi kwa watumiaji wengine wa barabara, kutoa maoni na kuripoti kuhusu tabia hatarishi) ya kisayansi, ya kisiasa, ya kihistoria, ya kifasihi,)
- kutumia kamusi kutafuta maana za maneno asiyoyajua
- kujenga rekodi ya msamiati aliojifunza katika kitabu
- kutunga sentensi akitumia msamiati katika matini aliyoisoma
- kusakura mtandaoni na kujichagulia matini ya ziada kisha aisome
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.5 Kusoma kwa Ufasaha
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- Kueleza vipengele vya kusoma kwa ufasaha ili kuvibainisha
- kusoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora
- kusoma kifungu kwa kasi ifaayo
- kusoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo
- kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo
- kuridhia kusoma makala kwa kuzingatia vipengele vinavyofanikisha mawasiliano
- Je, unaposoma kifungu unazingatia mambo gani ili kufanikisha usomaji?
- kujadiliana na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kusoma makala kwa ufasaha (matamshi bora, kasi ifaayo, sauti ifaayo, ishara zifaazo)
- kutazama vielelezo vya video za watu wanaosoma kwa ufasaha makala (k.v. hotuba, taarifa ya habari)
- kusoma kifungu kuhusu suala lengwa katika matini andishi au ya kidijitali akizingatia matamshi bora
- kusoma kifungu kuhusu suala lengwa kwa kuzingatia kasi ifaayo (maneno sahihi yasiyopungua 105 kwa dakika)
- kusoma kifungu akizingatia sauti ifaayo (k.v. kiwango cha sauti na kiimbo)
- kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo panapofaa (k.v. ishara za uso na mikono)
- kusoma mbele ya wenzake kazi yake ili wamtolee maoni
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.6 Kusoma kwa Kina Tamthilia Mbinu za Lugha
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua mbinu za lugha katika tamthilia
- kueleza umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika tamthilia
- kufurahia kuchanganua matumizi ya mbinu za lugha katika fasihi
- Tamthilia hutumia mbinu gani za lugha?
- Mbinu za lugha zina umuhimu gani katika tamthilia?
- kutambua mbinu za lugha kwenye tamthilia
- kueleza umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika tamthilia iliyoteuliwa na mwalimu
- kuhakiki uwasilishaji wa wenzake kuhusu mbinu za lugha katika tamthilia na kuutolea maoni
- kufanya utafiti maktabani au mtandaoni kuhusu matumizi ya mbinu za lugha katika tamthilia
- kuwasilishia mzazi au mlezi uchambuzi wa matumizi ya mbinu za lugha katika tamthilia aliyosoma
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.7 Kusoma kwa Ufahamu Kifungu cha Mjadala
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kudondoa habari mahususi katika kifungu cha mjadala
- kutambua msamiati mpya katika kifungu cha mjadala
- kuchambua mitazamo katika kifungu cha mjadala
- kuridhia kusoma kifungu cha mjadala ili kukuza uelewa wa habari
- Utawezaje kutambua habari mahususi katika hadithi unayoisoma?
- Je, unazingatia nini unaposoma vifungu vya ufahamu?
- kudondoa habari mahususi (k.v. nani, nini, wapi, lini) katika kifungu cha ufahamu cha mjadala
- kutambua msamiati mpya (k.v. maneno na nahau) katika kifungu cha ufahamu cha mjadala na kuueleza kwa kutumia kamusi
- kueleza maana ya msamiati uliotumiwa kwenye kifungu cha ufahamu cha mjadala na kutunga sentensi akiutumia
- kuchambua mitazamo iliyo katika kifungu cha ufahamu cha mjadala
- kuwawasilishia wenzake kazi yake ili waitolee maoni
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.8 Ufupisho
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza kwa usahihi ujumbe wa aya za matini kwa sentensi mojamoja
- kueleza kwa usahihi ujumbe wa aya zote za matini kwa aya moja
- kuandika ufupisho unaozingatia mtazamo wa matini ya kufupishwa
- kufurahia kufupisha ujumbe kwa usahihi katika miktadha mbalimbali
- Je, unazingatia nini unapofupisha kifungu cha ufahamu?
- kujadili vipengele vya ufupisho (k.v. habari muhimu katika aya, lugha ya anayefupisha, kudumisha mtazamo wa kifungu, idadi ya maneno)
- kueleza kwa usahihi ujumbe katika kila aya kwa kutumia sentensi mojamoja
- kueleza kwa usahihi ujumbe wa aya zote za matini kwa aya moja
- kujadili kuhusu jinsi ya kuandika ufupisho wa matini
- kuandika ufupisho unaozingatia mtazamo wa matini
- kumsomea mzazi au mlezi ufupisho alioufanya ili autolee maoni
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
