Kusikiliza na Kuzungumza
1.1 Kusikiliza na Kujibu Mahojiano
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika kusikiliza mahojiano
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika kujibu mahojiano
- kutumia vipengele vifaavyo katika kusikiliza na kujibu mahojiano ipasavyo
- kuchangamkia kushiriki mahojiano katika miktadha mbalimbali
- Je, ni vipengele vipi vinavyofaa kuzingatiwa katika kusikiliza mahojiano?
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika kusikiliza mahojiano
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika kujibu mahojiano
- kusikiliza mahojiano kuhusu suala lengwa katika kifaa cha kidijitali na kutambua vipengele vya kusikiliza na kujibu mahojiano vilivyozingatiwa
- kuwawasilishia wenzake vipengele vya kusikiliza na kujibu mahojiano vilivyozingatiwa katika mahojiano aliyosikiliza katika kifaa cha kidijitali
- kushiriki mahojiano kuhusu suala lengwa akiwa na wenzake, mzazi au mlezi kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya kusikiliza na kujibu mahojiano
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.2 Kusikiliza kwa Kina Sauti /g/ na /gh/
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua sauti /g/ na /gh/ katika silabi na maneno
- kutamka sauti /g/ na /gh/ ipasavyo katika silabi na maneno
- kutumia maneno yenye sauti /g/ na /gh/ ipasavyo katika matini ili kuyatofautisha kimatamshi
- kuchangamkia matamshi bora ya sauti /g/ na /gh/ katika mazungumzo ya kawaida
- Ni maneno yapi yaliyo na sauti /g/ na /gh/?
- kutambua sauti /g/ na /gh/ katika maneno na silabi
- kusikiliza maneno, sentensi au vitanzandimi vinavyohusisha sauti /g/ na /gh/ katika kifaa cha kidijitali na kutambua sauti hizo
- kutafuta maneno yenye sauti /g/ na /gh/ katika matini andishi au za kidijitali na kuyatamka ipasavyo
- kutunga sentensi akitumia maneno yenye sauti /g/ na /gh/ na kuziwasilisha darasani ili wenzake wazisikilize na kuzitathmini
- kushiriki mazungumzo na mzazi au mlezi wake kuhusu suala lengwa kwa kuzingatia matamshi bora ya sauti /g/ na /gh/
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.3 Hadithi Mighani
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza dhana ya mighani ili kuipambanua
- kujadili vipengele vya kuzingatia katika uwasilishaji wa mighani
- kujadili ujumbe na lugha katika mighani
- kusimulia mighani kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya uwasilishaji wa mighani
- kuchangamkia kushiriki katika uwasilishaji wa mighani katika miktadha mbalimbali ya kijamii
- Je, unaposimulia mighani unafaa kuzingatia vipengele gani?
- kutafiti na kueleza maana ya mighani
- kutafiri na kueleza sifa za mighani
- kujadili na wenzake vipengele vya kuzingatia katika uwasilishaji wa mighani
- kushiriki na wenzake kujadili ujumbe na lugha katika mighani aliyosikiliza ikitambwa na wenzake, mgeni mwalikwa au katika kifaa cha kidijiali kama vile kinasasauti
- kusikiliza mighani ikisimuliwa katika vifaa vya kidijitali au kutoka kwa mgeni mwalikwa na kubainisha sifa na vipengele vya uwasilishaji vilivyozingatiwa
- kusimulia mighani kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya uwasilishaji
- kuwasilishia mzazi, mlezi au mwenzake mighani aliyotafitia katika jamii yake na kujadili ujumbe husika
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.4 Hadithi Visasili
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza dhana ya visasili ili kuibanisha
- kujadili vipengele vya kimsingi katika uwasilishaji wa visasili
- kuwasilisha visasili kwa kuzingatia uwasilishaji ufaao
- kufurahia uchambuzi na uwasilishaji wa visasili ili kujenga umahiri katika fasihi simulizi
- Je, uwasilishaji wa hadithi ya visasili huzingatia vipengele gani?
- Visasili vina sifa gani?
- kutafiti na kueleza maana ya visasili
- kufanya utafiti maktabani na mtandaoni kuhusu sifa za visasili
- kuwawasilishia wenzake matokeo ya utafiti wake wa sifa za visasili ili wazijadili
- kujadili vipengele vya kimsingi katika uwasilishaji wa visasili (k.v. ujumbe, wahusika na mbinu za lugha)
- kusikiliza visasili katika vifaa vya kidijitali au kutoka kwa mgeni mwalikwa na kubainisha vipengele vya kimsingi vya uwasilishaji wa visasili
- kusimulia visasili kwa kuzingatia vipengele vya kimsingi vya visasili
- kujadili na mzazi au mlezi kuhusu visasili katika jamii yake
- kusimulia visasili akiwa na mzazi, mlezi au mwenzake akizingatia vipengele vya kimsingi vya uwasilishaji
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.5 Kusikiliza Maagizo
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya maagizo ili kuyapambanua
- kutambua maagizo katika miktadha mbalimbali
- kujadili sifa za kimsingi za maagizo yafaayo
- kutoa na kupokea maagizo ipasavyo
- kuchangamkia kutoa na kufuata maagizo ifaavyo katika miktadha mbalimbali
- Je, kwa nini mtu hupewa maagizo?
- Maagizo ambayo umewahi kupewa yalikusaidia vipi?
- kueleza maana ya maagizo ili kuipambanua
- kubainisha maagizo miongoni mwa kauli zilizoandikwa katika kadi, kapu maneno au vifaa vya kidijitali
- kutambua maagizo kutoka kwenye kitabu, chati au vifaa vya kidijitali
- kujadili na wenzake sifa za kimsingi za maagizo yafaayo
- kutafiti maktabani au mtandaoni kuhusu sifa za maagizo na kuwawasilishia wenzake darasani wazitathmini
- kuigiza utoaji na uitikiaji wa maagizo mbalimbali kwa uwazi
- kujadiliana na wenzake kuhusu aina mbalimbali za maagizo kulingana na miktadha ya jamii zao
- kusikiliza maagizo ya aina mbalimbali yanayotolewa na mwalimu, mgeni mwalikwa au katika kifaa cha kidijitali na kutaja maagizo yaliyomo
- kuandaa maagizo na kisha kuyawasilisha darasani ili yajadiliwe na wenzake
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.6 Kusikiliza kwa Kufasiri
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua ujumbe katika matini ya kusikiliza
- kueleza uhusiano kati ya ujumbe wa matini na maisha ya kila siku
- kujadili mafunzo yanayotokana na ujumbe wa matini
- kujenga mazoea ya kuhusisha ujumbe katika matini na hali ya maisha ya kila siku
- Ni ujumbe gani uliosikiliza katika matini ambao unafanana na mambo katika jamii yako?
- Unajifunza nini kutokana na ujumbe katika matini ulizosikiliza?
- kueleza masuala yanayozungumziwa katika matini aliyosikiliza kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au katika vifaa vya kidijitali
- kusikiliza matini katika vifaa vya kidijitali, kutoka kwa mwalimu au mgeni mwalikwa na kueleza uhusiano wa ujumbe wa matini hiyo na maisha ya kila siku
- kujadili na wenzake mafunzo yanayotokana na ujumbe wa matini
- kushirikiana na mzazi au mlezi kusikiliza na kuchanganua habari katika matini za aina mbalimbali kuhusu suala lengwa
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.7 Usikilizaji Husishi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya usikilizaji husishi ili kuubainisha
- kujadili vipengele vya kuzingatia katik a usikilizaji husishi
- kufanya mazungumzo yanayozingatia vipengele vya usikilizaji husishi
- kuchangamkia kushiriki katika usikilizaji husishi ili kujenga uhusiano mwema na wengine
- Unaposhiriki katika usikilizaji husishi, utazingatia nini ili kufanikisha usikilizaji?
- kueleza maana ya usikilizaji husishi akishirikiana na wenzake
- kujadili vipengele vya kuzingatia katika usikilizaji husishi
- kusikiliza mazungumzo kuhusu suala lengwa kutoka kwenye vifaa vya kidijitali akizingatia na kutambua vipengele vya usikilizaji husishi vilivyozingatiwa
- kumsikiliza mwenzake, mwalimu au mgeni mwalikwa akisema kauli au akisoma vifungu vifupi kuhusu suala lengwa na kufasiri hisia zake
- kuigiza kikao cha utoaji nasaha akishirikiana na wenzake huku akizingatia vipengele vya usikilizaji husishi
- kushiriki mazungumzo kuhusu suala lengwa na mzazi, mlezi au mwenzake huku akizingatia vipengele vya usikilizaji husishi
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.8 Uzungumzaji wa Papo kwa Hapo
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya uzungumzaji wa papo kwa hapo ili kuupambanua
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika uzungumzaji wa papo kwa hapo
- kutoa uzungumzaji wa papo kwa hapo kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya uzungumzaji
- kuchangamkia kutoa uzungumzaji wa papo kwa hapo ili kufanikisha mawasiliano
- Unazingatia mambo gani ili kufanikisha uzungumzaji wa papo kwa hapo?
- kueleza maana ya mazungumzo ya papo kwa hapo akishirikiana na wenzake
- kubainisha vipengele vya kuzingatia katika uzungumzaji wa papo kwa hapo
- kusikiliza uzungumzaji wa papo kwa hapo kuhusu suala lengwa yakitolewa na mwalimu, wenzake, mgeni mwalimu au kutoka kwenye vifaa vya kidijitali na kutathmini vipengele vya uwasilishaji vilivyotumika
- kushiriki katika uzungumzaji wa papo kwa hapo akizingatia vipengele vifaavyo
- kubuni uzungumzaji mwepesi wa papo kwa hapo kuhusu suala lengwa akizingatia vipengele vifaavyo na kuwawasilishia wenzake ili wautathmini
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.9 Kusikiliza kwa Kina
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua sauti /ch/ na /sh/katika silabi na maneno
- kutamka sauti /ch/ na /sh/ipasavyo katika silabi na maneno
- kutumia maneno yenye sauti /ch/ na /sh/ipasavyo katika matini ili kuyatofautisha kimatamshi
- kuchangamkia matamshi bora ya sauti /ch/ na /sh/katika mazungumzo ya kawaida ili kufanikisha mawasiliano
- Ni maneno yapi unayoyajua yaliyo na sauti /ch/ na /sh/?
- kutambua sauti /ch/ na /sh/katika maneno na silabi akishirikiana na wenzake
- kutambua maneno yenye sauti / ch/ na /gh/ katika matini andishi au za kidijitali na kuyatamka ipasavyo
- kutunga vitanzandimi vyenye maana akitumia sauti /ch/ na /sh/na kujirekodi kwa kutumia kifaa cha kidijitali
- kusikiliza na wenzake vitanzandimi alivyovirekodi ili kuvitathmini
- kumwasilishia mzazi au mlezi mazungumzo kuhusu suala lengwa kwa kuzingatia matamshi bora ya sauti /ch/ na /sh/
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.10 Hadithi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya hurafa na hekaya ili kuzibainisha
- kueleza ujumbe katika hurafa na hekaya
- kujadili vipengele vya uwasilishaji wa hurafa na hekaya
- kusimulia hurafa na hekaya kwa kuzingatia vipengele vya uwasilishaji
- kufurahia hurafa na hekaya kama vipera vya fasihi simulizi
- Je, hadithi ambayo umewahi kusikiliza ilihusu wanyama gani?
- Je, hurafa na hekaya hutofautianaje?
- kusikiliza kielelezo cha hadithi ya hurafa na hekaya kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au kifaa cha kidijitali
- kueleza maana ya hurafa na hekaya ili kuzibainisha akishirikiana na wenzake
- kueleza ujumbe katika hurafa na hekaya
- kujadili na mwenzake vipengele vya uwasilishaji wa hurafa na hekaya
- kuwasilisha hurafa na hekaya kwa kuzingatia vipengele vya uwasilishaji (kiini cha hadithi, kiwango cha lugha, mpangilio wa matukio, sauti, ishara za mwili)
- kujirekodi akitamba hurafa na hekaya kwa kutumia vifaa vya kidijitali na kusikiliza
- kushirikiana na mzazi au mlezi kutambua hurafa na hekaya kutoka kwa jamii yake na kujadili ujumbe unaojitokeza katika hadithi hizo
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.11 Kuzungumza kwa Kutumia Vidokezo vya Hoja
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua umuhimu wa kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja
- kutambua miktadha katika jamii ambapo kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja hufanywa
- kujadili vipengele vya kuzingatia katika kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja
- kutoa mazungumzo kwa kutumia vidokezo ifaavyo
- kujenga mazoea ya kutumia vidokezo katika mazungumzo ili kufanikisha mawasiliano
- Kwa nini ni muhimu kuandaa vidokezo unapozungumza?
- kueleza maana ya kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja
- kujadili na wenzake umuhimu wa kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja
- kutambua miktadha katika jamii yake ambamo anahitaji kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja
- kujadili na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kuzungumza kwa kutumia vidokezo vya hoja
- kusikiliza au kutazama aina mbalimbali za mazungumzo kutoka kwenye vifaa vya kidijitali, mgeni mwalikwa au wenzake na kubainisha vipengele vilivyozingatiwa
- kuandaa vidokezo kuhusu suala lengwa
- kuwawasilishia wenzake mazungumzo kuhusu suala lengwa kwa kutumia vidokezo alivyoandaa ili wayatolee maoni
- kumwasilishia mzazi au mlezi vidokezo vya mazungumzo kuhusu suala lengwa ili atoe maoni yake
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.12 Kusikiliza kwa Makini
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza habari katika matini ya kusikiliza
- kukadiria maana ya msamiati mahususi na vifungu katika matini ya kusikiliza
- kudondoa habari muhimu katika matini aliyosikiliza kwa kufuata mpangilio ufaao
- kujenga mazoea ya kufurahia kusikiliza vifungu vya kusikiliza ili kuimarisha uwezo wa kusikiliza
- Je, kwa nini ni muhimu kuwa na mpangilio ufaao wa hoja kutoka habari uliyosikiliza?
- kusikiliza matini kutoka kifaa cha kidijitali au mwalimu wake
- kutambua hoja muhimu katika habari aliyosikiliza kuhusu suala lengwa kutoka kwa mwalimu, kifaa cha kidijitali, mgeni mwalikwa au wenzake
- kueleza hoja muhimu aliyotambua kutoka matini aliyosikiliza
- kukadiria maana ya msamiati mahususi na vifungu katika matini aliyosikiliza
- kuelezea mwenzake maana ya msamiati katika matini ya kusikiliza
- kudondoa habari muhimu katika matini aliyosikiliza kwa kufuata mpangilio ufaao
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.13 Hadithi Wahusika
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua wahusika katika hadithi
- kuchambua sifa za wahusika katika hadithi
- kueleza mafunzo kutokana na wahusika katika hadithi
- kufurahia kushiriki katika uchambuzi wa wahusika katika hadithi
- Je, hadithi uliyowahi kusimuliwa ilikuwa na wahusika gani?
- kutambua washiriki katika hadithi inayosimuliwa (k.v. fanani, hadhira)
- kutambua wahusika katika hadithi inayosimuliwa
- kutambua sifa za wahusika katika hadithi aliyosikiliza kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au vifaa vya kidijitali
- kuchambua wahusika katika hadithi aliyosikiliza
- kueleza mafunzo kutokana na wahusika katika hadithi
- kutamba hadithi akiwa na wenzake huku wakichukua majukumu mbalimbali (k.v. fanani, hadhira)
- kutunga hadithi fupi ambayo ina wahusika wanyama kuhusu suala lengwa na kuwawasilishia wenzake darasani ili wachambue wahusika
- kuwasilishia mzazi au mlezi uchambuzi wa sifa za wahusika katika hadithi aliyosikiliza
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.14 Hadithi Matumizi ya Lugha
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua vipengele vya lugha vinavyotumika katika hadithi
- kujadili umuhimu wa vipengele vya lugha vinavyotumika katika hadithi
- kusimulia hadithi kwa kutumia vipengele vya lugha ipasavyo
- kuonea fahari uchanganuzi wa lugha katika hadithi kama utungo wa fasihi simulizi
- Ni mbinu gani za lugha zinazotumika katika masimulizi ya hadithi?
- Matumizi ya lugha katika hadithi yana umuhimu gani?
- kutambua vipengele vya lugha kwa kusikiliza hadithi kutoka kwa mwalimu au vifaa vya kidijitali
- kujadili umuhimu wa vipengele vya lugha vilivyotumika katika hadithi walizosikiliza
- kusimulia hadithi kwa kutumia vipengele vya lugha
- kuwawasilishia wenzake hadithi aliyotunga ili watambue vipengele vya lugha vilivyotumika
- kushirikiana na mzazi au mlezi kusikiliza hadithi na kutambua vipengele vya lugha vilivyotumika
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.15 Usikilizaji Husishi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kueleza maana ya usikilizaji husishi
- kutambua vipengele vya usikilizaji husishi katika matini
- kujadili vipengele vya usikilizaji husishi ili kuvipambanua
- kushiriki mazungumzo akizingatia vipengele vya usikilizaji husishi
- kuchangamkia kushiriki katika kusikiliza husishi ili kuimarisha uwezo wa kufuatilia habari zinazoelezwa
- Je, ni miktadha gani rasmi na isiyo rasmi ambapo usikilizaji husishi hutokea?
- Ni vipengele gani unazingatia katika kusikiliza husishi?
- kueleza maana ya usikilizaji husishi
- kutambua miktadha rasmi na isiyo rasmi ambamo kusikiliza husishi hutokea katika jamii yake
- kutambua vipengele vya kuzingatia katika kusikiliza husishi (k.v. kuwa makini, kuuliza maswali yasiyoelekeza, kuomba ufafanuzi, kumtazama mzungumzaji, kuelewa ujumbe anaotaka kukupitishia, kumhimiza kuzungumza badala ya kutoa ushauri, kutumia ishara zifaazo) kutoka kwenye mazungumzo mafupi
- kusikiliza mazungumzo kuhusu suala lengwa kutoka vifaa vya kidijitali kama vile vinasasauti na akizingatia, na kutambua vipengele vya kusikiliza husishi vilivyozingatiwa
- kuigiza vikao rasmi vya mazungumzo, (k.v. kati ya mwalimu mkuu na mzazi kuhusu nidhamu ya mtoto) akishirikiana na wenzake
- kujadili vipengele vya kusikiliza husishi vilivyozingatiwa na wahusika katika mazungumzo hayo
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
