Lishe Bora
1.1 Msamiati
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua msamiati kuhusu lishe bora ili kuimarisha mawasiliano
- kusoma maneno yanayohusiana na lishe bora ili kuimarisha usomaji
- kuandika maneno yanayohusu lishe bora katika kuimarisha uandishi bora
- kutumia msamiati ulisomwa katika kutunga sentensi ili kuimarisha mawasiliano
- kuthamini kula chakula kinachofaidi mwili ili kujikinga kutokana na madhara ya ukosefu wa lishe bora.
- Je, unaweza kutambua vyakula vipi?
- Ni chakula kipi unachokipenda?
- Ni chakula kipi kinachofaidi mwili zaidi?
- Ni chakula kipi kinachodhuru afya?
- Mwanafunzi aelezee maana ya msamiati unaohusiana na lishe bora kama vile protini, vitamini, wanga (vyakula vinavyopatia mwili nguvu) chumvi, ukosefu, upungufu na baadhi ya vyakula vinavyofaidi mwili na afya.
- Wanafunzi wajadiliane katika vikundi au wakiwa wawili wawili kuhusu vyakula vinavyodhuru afya.
- Mwanafunzi atazame kwenye vyombo vya kiteknolojia na kuvijadili picha za vyakula vinavyoashiria msamiati unaorejelewa.
- Mwanafunzi asome majina mbalimbali ya vyakula kwenye kadi za maneno.
- Mwanafunzi anakili kwenye daftari msamiati unaofunzwa.
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.2 Kusikiliza na Kuzungumza: Masimulizi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kutambua vyakula vinavyofaa mwili ili kuimarisha stadi ya kuzungumza
- kuzungumzia juu ya chakula anachokipenda ili kuimarisha mazungumzo
- kuzungumzia juu ya chakula kinachodhuru afya ili kuelewa madhara ya vyakula hivyo
- kusikiliza masimulizi kuhusu lishe bora ili kujenga stadi ya kusikiliza
- kuthamini vyakula vinavyofaidi mwili ili kuchagua vyakula kwa uangalifu.
- Unapenda kula chakula gani?
- Chakula unachokila husaidiaje mwili?
- Ni chakula kipi kinachoweza kudhuru afya?
- kikiliwa sana?
- Mwanafunzi ataje baadhi ya vyakula kwa kuonyeshwa michoro na vyakula halisi.
- Wanafunzi wajadiliane kuhusu umuhimu wa vyakula mbalimbali k.m. vinavyompa mtu nguvu, vinavyomkinga mtu kutokana na magonjwa, vinavyoleta joto mwilini, vinavyowezesha mtu kukua n.k.
- Mwanafunzi ashiriki katika mazungumzo kuhusu
- chakula akipendacho.
- Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu chakula kinachodhuru afya k.m. vibanzi, biskuti
- Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akisimulia kuhusu lishe bora na madhara ya vyakula vinavyodhuru afya
- Mwanafunzi aweza kuonyeshwa video kuhusu lishe bora na madhara ya vyakula hasi na baadaye washiriki katika mijadala ya vikundi.
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.3 Kusoma: Hadithi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- kusikiliza hadithi ya mwalimu ili kuimarisha stadi za kusikiliza na kusoma
- kusoma hadithi kwa mtiririko ufao ili kuimarisha stadi ya kusoma
- kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa ili kuelewa ujumbe katika hadithi
- kuchangamkia kusoma hadithi ili kuendelea kujenga stadi ya kusoma.
- Ni hadithi zipi ambayo umewahi kusoma?
- Ni hadithi ipi iliyokufurahisha zaidi?
- Unamkumbuka nani katika hadithi hiyo?
- Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
- Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
- Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
- Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi, asome pamoja na mwalimu kisha asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kupitia kinasasauti.
- Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma na kusomewa hadithi.
- Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu au mtoto akisoma hadithi husika kwa ufasaha kisha aige usomi ule.
- Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi.
- Mwanafunzi asimulie hadithi kutokana na picha alizopewa kuhusu lishe bora.
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
1.4 Sarufi:Matumizi ya hiki na hivi
By the end of this sub-strand, the learner should be able to:
- aweze:
- Unatumia neno gani kuonyeshea?
- Mwanafunzi asome vifungu vinavyojumuisha hiki na hivi kama vile Kitabu hiki – Vitabu hivi; Kiti hiki –
Approved textbooks, realia, counters, flashcards, charts & digital devices.
